Habari

Waziri Kapinga Atembelea Baraza la Ushindani
  • 02 Dec, 2025
Waziri Kapinga Atembelea Baraza la Ushindani

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith S. Kapinga, ametembelea Baraza la Ushindani (FCT) leo tarehe 25 Novemba 2025 katika ofisi za Baraza zilizopo Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo, Mhe. Kapinga alipokea taarifa kuhusu namna Baraza linavyotekeleza majukumu yake chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara, ikiwemo usimamizi wa mashauri ya ushindani na juhudi za kulinda maslahi ya watumiaji wa bidhaa na huduma nchini.

Mhe. Kapinga pia amelipongeza Baraza la Ushindani (FCT) kwa kufanikiwa kukuza na kulinda ushindani wa haki sokoni.

Aidha, Waziri Kapinga ameahidi kutoa ushirikiano wa dhati ili kuhakikisha Baraza linafanikiwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo katika kuinua uchumi wa nchi.

Ziara hiyo imetoa mwanga mpya kuhusu uwezo, wajibu, na mwelekeo wa Baraza katika kukuza ushindani wa haki na kuimarisha mazingira bora ya biashara nchini.