Muundo wa Baraza
Muundo wa Baraza
Baraza linaundwa na Mwenyekiti na Wajumbe sita.
Mwenyekiti ambaye anapaswa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu huteuliwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kushauriana na Jaji Mkuu chini ya kifungu cha 83(2)(a) cha Sheria ya Ushindani, 2003.
Wajumbe pia huteuliwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kushauriana na Mwanasheria Mkuu na wanatokana na mapendekezo ya Kamati maalum. Wajumbe huteuliwa kwa kuzingatia vigezo vya kuwa na ufahaumu wa, au uzoefu katika sekta, biashara, uchumi, sheria au utawala chini ya kifungu cha 83(2)(b) cha Sheria ya Ushindani, 2003.
Mwenyekiti na Wajumbe hutekeleza majukumu ya kimahakama na kutumikia Baraza pale wanapohitajika yaani “on part time basis” kwa kipindi cha miaka mitatu na huweza kuongezewa miaka mitatu mengine.
Majukumu ya kiutawala ya Baraza kutekelezwa na Msajili ambaye huteuliwa na Mh. Waziri wa Viwanda na Biashara baada ya kushauriana na Jaji Mkuu chini ya kifungu cha 86 cha Sheria ya Ushindani, 2003. Msajili anasaidiwa na watumishi wengine wa ngazi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Idara na maafisa.