Karibu

Karibu Baraza la Ushindani

Karibu Baraza la Ushindani!

Mwenyekiti, Wajumbe, Menejimenti na Watumishi wa Baraza la Ushindani (FCT) wanawakaribisha kwenye tovuti ya FCT. 

FCT ni "specialist quasi judicial body"  kinachosikiliza na kuamua mashauri ya rufaa yanayohusiana na maswala ya ushindani na udhibiti wa soko. Ni chombo muhimu kwenye mfumo wa ushindani na udhibiti wa soko, mfumo ambao unahakikisha ukuaji wa uchumi wa wananchi wa Tanzania na uchumi wa Taifa kwa ujumla kwa kudhibiti soko na kuleta ushindani katika soko ili kumlinda mlaji kutokana na mienendo mibaya sokoni, kuleta ufanisi, kusaidia uvumbuzi na kuleta maendeleo endelevu.

Tovuti hii ina lengo la kuhabarisha na kuelimisha Umma kuhusu shughuli zinazofanywa na FCT. Ni imani yangu kuwa Tovuti hii itakuwa na manufaa kwa wageni wetu.

Karibuni sana!