Habari

ORIENTATION SEMINAR FOR CAPACITY BUILDING TO FAIR COMPETITION TRIBUNAL MEMBERS HELD IN ARUSHA
  • 07 Sep, 2026
ORIENTATION SEMINAR FOR CAPACITY BUILDING TO FAIR COMPETITION TRIBUNAL MEMBERS HELD IN ARUSHA

Translate in english Semina elekezi kwa Baraza la Ushindani (FCT) ikishirikiana na Tume ya Ushindani (FCC) imefanyika mnamo tarehe 06 Agosti, 2025 jijini Arusha kwa mafanikio makubwa, ikilenga kuwajengea uwezo Wajumbe wa Baraza kuhusu namna bora ya kushughulikia rufaa zinazohusiana na masuala ya ushindani wa kibiashara na udhibiti wa Soko nchini.

Mgeni rasmi katika Semina hiyo alikuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhe. Needpeace J. Wambuya, ambaye alifungua rasmi Semina hiyo huku akisisitiza umuhimu wa Baraza hilo katika kukuza uchumi wa Taifa letu.

“Baraza la Ushindani lina nafasi muhimu sana katika kuhakikisha haki inatendeka kwa upande wa rufaa zinazohusiana na ushindani wa kibiashara na udhibiti wa Soko. Kupitia utendaji wake wa haki na wa haraka, Baraza lina mchango mkubwa katika kuimarisha mazingira ya biashara na uchumi kwa ujumla nchini,” alisema Mhe. Wambuya. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani, Mhe. Jaji Rose Ally Ebrahim, alieleza kuwa Semina hiyo inalenga kuwawezesha Wajumbe wa Baraza kutoa maamuzi kwa ufanisi zaidi.

“Tunayahitaji maarifa haya ili kuelewa kwa undani namna Tume na Mamlaka za Udhibiti mbalimbali husika zinavyotekeleza majukumu yao, hasa tunaposhughulikia rufaa zinazohusu ushindani na udhibiti wa Soko,” alieleza Jaji Ebrahim.

Naye Msajili wa Baraza hilo, Mhe. Wema Mbegu Kaskasi, alieleza kuwa Baraza limejipanga kusikiliza mashauri 32 mwezi huu wa Agosti na kwamba juhudi zinafanyika kuharakisha utoaji wa maamuzi kwa wakati.

“Tunamshukuru sana Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uteuzi wa Mwenyekiti wetu, Mhe. Jaji Rose Ally Ebrahim, pamoja na Wajumbe sita wa Baraza hili muhimu,” alisema Kaskasi. Katika Hotuba yake,

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), Bi. Khadija Ngasongwa, alieleza kuwa ushirikiano kati ya FCC na FCT ni wa msingi hasa katika kushughulikia rufaa. Semina hiyo imeonekana kuwa hatua muhimu katika kuimarisha utendaji wa Baraza la Ushindani, huku matarajio yakiwa ni kuongeza ufanisi, uwazi na haki katika masuala ya ushindani wa kibiashara na udhibiti wa Soko nchini.

slot gacor